Ushauri wa kiafya ambao WHO imeeleza ni imani potofu, kuhusu kutibu virusi vya corona


Virusi vya corona vimeonekana kuenea katika nchi nyingi zaidi duniani na mpaka sasa ugonjwa huo tiba yake haijapatikana.



Hata hivyo kukosekana kwa tiba hiyo hakujawafanya watu kuacha kutafuta ushauri wa kitabibu kuanzia kwenye tiba ambazo hazina madhara mpaka zile ambazo ni hatari kwa afya zao.

Ushauri wa kiafya ambao umeenea kwa kasi mtandaoni ambao hauna uhusiano na kile ambacho sayansi wanachosema.

1. Vitunguu saumu

Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wanashauri watu kula vitunguu swaumu ili kuzuia kupata maambukizi ya corona.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa vyakula kwa afya mara nyingine huwa vina vimelea ambavyo si salama kwa binadamu, Hakuna uthibitisho unaosema kuwa mtu akila kitunguu swaumu basi anaweza kujilinda na virusi vipya vya corona.

Katika kesi nyingi, aina hii ya tiba huwa haina madhara makubwa kwa afya kama watu wanazingatia utaratibu wa kiafya ambao au kufuata ushauri wa daktari.

Lakini wanapaswa kufahamu uwezo wa kile wanachoambiwa.

Huko Kusini mwa China, taarifa zimeripoti kuwa kuna mwanamke ambaye alipaswa kupata huduma za kiafya hospitalini alitumia vitunguu swaumu vibichi kilo moja na nusu.

Tunafahamu kwa ujumla kuwa kula matunda na mboga za majani pamoja na kunywa maji kunaweza kukufanya mtu uwe na afya njema.

Ingawa hakuna ushahidi unaosema kuwa chakula fulani ni tiba na kinaweza kupambana na virusi vya aina fulani.

2. ‘Madini‘

Mmiliki wa YouTuber Jordan Sather, ambaye ana maelfu ya wafuasi kutoka duniani kote amekuwa akidai kuwa kuna madini ya miujiza ambayo yanaweza kuponya virusi vya corona.

Hii inajumuisha watengeneza dawa aina ya ‘chlorine dioxide’ ambayo iliweza kutibu kansa.

Presentational white space
Mwaka jana Mamlaka ya chakula na dawa Marekani imetoa angalizo kuhusu hatari za kiafya.

Mamlaka za afya katika mataifa mengine pia wametoa angalizo kuhusu jambo hilo.

Mamlaka hiyo imedai kuwa haijapata utafiti wowote ambao unaonyesha kuwa kuna vitu ambavyo vinaweza kutibu ugonjwa wowote.

Imetoa angalizo kuwa kunywa dawa hizo ambazo hazijathibitiwa kunaweza kusababisha kichefuchefu, kutapika, kuharisha na dalili za kuishiwa maji.

Presentational white space
Sign says hand sanitiser is out of stock
3. Dawa ya kuoshea mikono iliyotengenezwa majumbani

Kumekuwa na ripoti nyingi za kudai kuwa dawa za kuoshea mikono zimeisha , wakati kuosha mikono ndio jambo muhimu watu wameambiwa kuzingatiwa ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

Ripoti za upungufu wa dawa hizo zilianza kujitokeza nchini Italia, hivyo watu walianza kufundisha namna ya kutengeneza dawa hizo nyumbani kupitia mtandao wa kijamii.

Lakini mahitaji ya kutengeneza dawa hizo, wanasayansi wamedai kuwa si salama kwa matumizi ya kwenye ngozi.

Kilevi kutengeneza dawa ya kuoshea mikono nyumbani si jambo sahihi.

Profesa Sally Bloomfield, kutoka chuo cha afya amesema kuwa haamini kuwa pombe inawezi kutengeneza dawa za kuoshea mikono.

4.Kinywaji cha madini ya fedha

Wazo la matumizi ya kinywaji cha madini ya fedha ambacho kilianzishwa na mchungaji wa Marekani Jim Bakker kilikatazwa kutokana.

Madani ya kinywaji cha madini hayo kuwa suluhisho la maambukizi ya virusi vya corona ndani ya saa 12, ingawa amekubali kuwa hajawahi kutumia kkwa mtu mwenye virusi vya corona.

Wazo hilo lilienea kwenye mtandao wa facebook kuwa kinywaji hicho kinaweza kutibu virusi vya corona.

5. Kunywa maji kila baada ya dakika 15

Picha moja ilisambaa katika mtandao wa Facebook ikimnukuu daktari wa Japan kuwa mtu akinywa maji kila baada ya dakika 15, anakuwa anasafisha mwili hivyo anajikinga na maambukizi ya virusi.

Na maelezo mengine ya aina hiyo yalishirikishwa kwenye mtandao zaidi ya mara 250,000.

Professa Trudie Lang kutoka chuo kikuu cha Oxford alisema kuwa hakuna uhusiano wowote wa kibaiolojia ambao unahusisha wazo hilo kuwa kunywa maji mengi kunaweza kukua vijijidudu vya corona.

Maambukizi ya kama ya corona yakiingia kwenye mwili yanaweza kuambukizwa kwa mtu kuhema. Baaadhi ya maambukizi yanaweza kupita kwenye kinywa hivyo hata ukinywa maji huwezi kuzuia.

6. Joto ali na kujizuia kula barafu

Watu wamekuja na ushauri wa kila aina, wengine wakidai kuwa joto linauwa virusi hivyo na kuwashauri watu wanywe maji ya moto , kuoga maji ya moto .

Ushauri ambao ulichukuliwa na na watu wengi katika mitandao ya kijamii katika nchi mbalimbali na kudaiwa kuwa Unicef wamethibitisha wakati ni uongo, walidai kuwa kunywa maji ya moto na kukaa kwenye jua na kujizuia kula barafu.

Presentational white space
Unicef ilitoa angalizo kwa watu kuwa makini na taarifa ambazo si sahihi , hakuna ukweli kuwa ‘ice cream'(barafu) na vyakula vya baridi vinaweza kuzuia mtu kupata magonjwa.

Huo ni uongo kabisa.

Tunafahamu kuwa virusi vya mafua huwa havikali kwenye mwili wakati wa jua lakini hatufahamu kama virusi vipya vinaweza kudhurika na jua.

Kujaribu kukaa kwenye jua wakati virusi viko tayari kwenye mwili wako, hakuna namna ambayo jua linaweza kukabiliana na virusi hivyo, kwa mujibu wa Profesa Bloomfield.

Kuoga maji ya moto au kunywa maji ya moto hakutaweza kuuwa vijijidudu wakati ukiwa mgonjwa tayari.



Chanzo BBC
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad