MKALI wa muziki Afrika, raia wa Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ amethibitishia kuwa ameendelea kupishana na mlipuko wa Virusi vya Corona, baada ya kufanyiwa vipimo mara mbili na kukutwa yupo mzima na wala hana maambukizi.
Davido alichukua uamuzi wa kupima na kujitenga peke yake, mara baada ya mchumba na mama mtoto wake, Chioma kukutwa na maambukizi ya Corona aliyoyapata nchini England, huku yeye akirejea Nigeria akitokea nchini Marekani alikokatisha ziara yake ya muziki kwa sababu ya kusambaa kwa virusi hivyo.
Davido alitoa taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter kwa kuandika: “Nimefanya vipimo vya Covid-19, nimekutwa nikiwa mzima tena, hata Chioma naye yupo vizuri hajaonyesha utofauti wa afya yake.”
Davido bado yupo karantini akijiangalia hali yake kwa siku 14 baada ya kurudi kutoka nchini Marekani.