Diamond Aomba Msamaha Kwa Zari "Tutapanga Jinsi ya Kuwalea Watoto Wetu"



Huku janga la virusi vya corona likizidi kuwa tishio kote duniani, kila taifa limebuni njia mbali mbali ya kuwasadia wasiojiweza katika jamii haswa baaa ya wengi kukosa ajira.

Msanii Diamond Platnamz ni kati ya wathamini waliojitokeza kuonyesha wema kwa wasiojiweza msimu huu wa Ramadhan, akiahidi kulipa kodi ya nyumba kwa familia 500.

Ahadi yake hii ilimuamsha mpenziwe wa zamani Zari aliyemshambulia kwa kuweka ahadi za uongo kwa umma.


Kulingana na Zari, Diamond hawezi kujifanya kuwa ataweza kuzisaidia familia 500 katika kuzilipia kodi ya nyumba wakati ameshindwa kukidhia mahitaji ya familia yake. Ujumbe wake ukimuanika msanii huyu kuhusu jinsi alivyowatelekeza wanawe.

…….na hujui wanachokula wanao, ma hata jinsi wanavyolala, ama iwapo bima ya hospitali na karo kulipwa. Hutaweza kufurahisha ulimwengu wakati wanao hawana furaha. Unaeneza uongo….,’’ Ujumbe wa Zari.


Akihojiwa katika redio ya Wasafi asubuhi ya Jumatatu, Aprili, 27 kuhusu jinsi msaada wake ungefika kwa familia hizo, msanii huyu alieleza pia kuwa aliona ujumbe wa Zari mtandoni na kuchukua fursa ya kipekee kumpigia simu wakazungumza na.

Alieleza kuwa anamheshimu Zari na Licha ya tofauti zao yuko tayari kuwalea wanawe.


‘’Baada ya kuona ujumbe ule waZari, nilimpigia simu na kumueleza, licha ya tofauti zetu ila bado na mamheshimu sana. Alienielewa na nadhani baada ya corona kuisha tutapanga namna ya kuwalea watoto wetu pamoja,’’ Diamond alisema.

Inadaiwa kuwa ujumbe wa Zari ulikuwa umemtia wasiwawi Tanasha baada ya kupata habari kuwa Mondi hashughuliki katika kuwalea wanawe, Dona akiachiwa jukumu la kumlea mwanawe kivyake. Ujuembe wa Mondi kwa Zari huenda utampa tumaini tena.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad