Diamond na Harmonize Wampe Somo Ali Kiba



tHuu ni ukweli unaomiza tumeshamuona Diamond akipiga hatua kumi mbele ya Alikiba akaja akamtoa kijana Harmonize ambaye nae amepiga hatua tano mbele kwa Alikiba.

Hapa nazungumzia hatua za kimuziki, shows, mauzo ya nyimbo kwenye platform mbalimbali tukiende kwa Diamond yeye ameenda mbele zaidi kwakua mfanyabiashara anayemiliki online media, radio station, television na pia kampuni ya utengenezaji video Zoom extra.

Kwenye masuala ya kuwa balozi kwenye makampuni makubwa Diamond yupo mbele zaidi akifuatiwa na Harmonize ambaye yeye ni balozi wa makampuni ya Sayona drinks na leo ametangazwa kuwa balozi wa CRDB bank .

Ushauri wangu kwa Alikiba inabidi ajifunze kwa hawa vijana wenzake tena ikibidi akaombe darasa apigwe msasa yeye na mameneja wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad