Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dk Faustine Ndugulile, amesema mama mwenye maambukizi ya Covid-19 anapaswa kuendelea kunyonyesha mtoto wake.
“Hakuna ushahidi kuwa maziwa yanaambukiza Corona,” aliandika Dk Ndugulile.
“Kuvaa barakoa kipindi chote cha unyonyeshaji, usafi wa mwili kabla ya kunyonyesha na usafi wa matiti na mikono kabla ya kunyonyesha,” aliandika Dk. Ndugulile katika ukurasa wake wa Twitter
Mama mwenye maambukizi ya Covid-19 anapaswa kuendelea kunyonyesha mtoto wake. Hakuna ushahidi kuwa maziwa yanaambukiza Corona. Zingatia:— Faustine Ndugulile (@DocFaustine) April 22, 2020
1. Kuvaa barakoa kipindi chote cha unyonyeshaji.
2. Usafi wa mwili kabla ya kunyonyesha
3. Usafi wa matiti na mikono kabla ya kunyonyesha.