KIMENUKA..Dudubaya Aitwa Tena Kuhojiwa BASATA
1
April 13, 2020
BARAZA la Sanaa laTaifa (Basata) limemwandikia barua mwimbaji maarufu nchini, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya‘ ili kujieleza kutokana na kutumia lugha isiyo ya staha kwenye mitandao ya kijamii.
Dudubaya anatakiwa kuripoti kesho Jumanne kwenye ofisi za makao makuu ya baraza hilo. Mwimbaji huyo ameiposti barua hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram na kukubali wito huo siku ya Jumanne.
Inaelezwa kuwa, BASATA wamemwita Dudubaya kutokana na kuvujisha video aliyojirekodi akimtukana matusi ya nguoni Mwendeshaji wa Mashindano ya Kusaka Vipaji vya Muziki, Bongo Star Search (BSS), Ritha Paulsen ‘Madam Ritha’ akidai kuwa amekuwa akiwadhulumu wasanii.
Aidha, katika clip hiyo ya video iliyosambaa mitandaoni inamwonyesha Dudubaya akiwatukana wanahabari na baadhi vya vyombo vya habari kwa madai kuwa wamelipwa pesa ili wasiripoti tukio la Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alipokuwa akizungumza na wanahabari kuhusu BSS kutomlipa mshindi wa shindano hilo kwa mwaka 2019.
Tags
Basata, Konki alicho zungumza ni cha kweli.
ReplyDeleteKutokana na Uchungu wa Kuwa Dhulumu hawa Vijana chipukizi Wanyonge.
Hata Mimi Ningezungumza kwa Jazba kuliko hivyo.
Yte tisa. Mada na Uhalisia Vinaeleweka
washindi wote kuanzia 2013 muwaite kuchukua malalamiko na Mkkubwa pia,kabla hamaifungia Bench Mark na atimae kulipa haki walizo Dhulumu.