Emirates yazindua Vipimo vya Muda Mfupi vya Corona



Shirika kubwa la ndege ulimwenguni la Emirates, limezindua kipimo cha virusi vya corona kinachotoa majibu katika muda wa dakika kumi na maalumu kwa ajili ya abiria wake wanaosafiri kutokea uwanja wake wa nyumbani ulioko Dubai.

Shirika hilo limesema kipimo hicho ni cha kwanza kuzinduliwa katika sekta ya usafiri wa anga. Shirika hilo limerejesha safari zake za ndege za abiria mapema mwezi huu baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu kusimamisha safari zake zote za kibiashara.

Hata hivyo safari hizo hazitawahusu abiria kuingia nchini humo kutoka mataifa mengine.

Kipimo hicho cha damu kilijaribiwa na waziri wa afya wa Dubai katika kituo cha ukaguzi na matokeo kutoka baada ya dakika kumi.

Waziri huyo amesema kipimo hicho kitawezesha kutoa majibu ya haraka kwa abiria wa ndege zake wanaokwenda kwenye mataifa yanayotaka vyeti vya vipimo vya COVID-19.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad