Erick Shigongo Awafungukia Madaktari Wanaotibu Wagonjwa wa Corona "Laiti Tungefahamu ni Kiasi Gani Wanateseka na Wakati Mwingine Kupoteza Uhai"

Shukrani nyingi kwa madaktari na Wauguzi wetu.
Wiki mbili zilizopita rafiki yangu mmoja alilazwa hospitali, awali alipopimwa aligundulika kuwa na malaria, akaanza matibabu bila nafuu, baadae ndipo akagundulika tena kuwa na Corona!

Karibu madaktari na wauguzi wote waliomhudumia walichukuliwa ma kuwekwa karantini!!!!!!! Maisha yao
Wakawa yameingia hatatini wakijaribu kuokoa maisha ya rafiki yangu.

Kila ninapowafikiria ndugu zetu wauguzi na Madaktari kwa kweli nakosa maneno ya kusema kuelezea shukrani za moyo wangu kwao, wakati sisi tumelala wao wanatia maisha yao hatarini kwa ajili yetu na ndugu zetu katika kipindi hiki kigumu cha ugonjwa wa Corona.

Huko Italia na Marekani idadi kubwa ya wauguzi na Madaktari wamepoteza uhai wao baada ya kuambukizwa ugonjwa wa Corona wakijaribu kuokoa maisha ya watu wengine, huu ni upendo wa Agape, usio na masharti.
Swali la kujiuliza je wanalipwa
Kwa kuhatatarisha maisha yao kiasi hiki?

Laiti tungefahamu ni kiasi gani wanateseka na wakati mwingine kupoteza uhai kwa ajili yetu hakika tungewaombea, kuwapongeza, kuwashukuru, kuwajali na kuwapigia makofi ya nguvu bila kukoma, hatuwalipi kiasi cha kuhatarisha masiha yao lakini hawaachi kazi kila siku wanakwenda kazini hata kama wenzao wanaambukizwa na kuwekwa karantini na kufa.
Jambo moja la muhimu sana ambalo wauguzi wanapaswa kulifahamu ni kwamba wanao wajibu wa kulinda maisha yao wawapo kazini, pia serikali inao wajibu wa kuwapa vitendea kazi vya kuhakikisha wapo salama wakati wote, vinginevyo ipo siku itajikuta madaktari ma wauguzi wake wote wapo Karantini na hakutakuwa na mtu wa kuhudumia wagonjwa!

ASANTENI MADAKTARI, ASANTENI WAUGUZI NA WAHUDUMU WOTE WA AFYA MUNGU
ATAWALIPA KWA KAZI NJEMA MNAYOLIFANYIA TAIFA HILI NA WATU
WAKE 🙏🏼🇹🇿 Asanteni na Mungu awabariki.
Eric Shigongo James,
Mwandishi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad