Gabon Wamtaka Aubameyang Aondoke Arsenal




RAIS wa Shirikisho la Soka la Gabon (Fegafoot), Pierre Alain Mounguengui, amemshauri straika Pierre- Emerick Aubameyang kujiunga na timu yenye shauku ya makombe kuliko Arsenal.

 

Aubameyang amejitengenezea sifa ya kuwa mmoja wa mastraika hatari zaidi tangu alipotua Arsenal akitokea Borussia Dortmund Januari 2018, na amebakiza bao moja tu afikishe mabao 50 Premier.

 

Hata hivyo, licha ya kufunga mabao mengi kiasi hicho, timu yake haijafanikiwa kutwaa kombe lolote tangu atue huku akiwa pia hajafanikiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na timu hiyo.

 

“Arsenal haina shauku kama timu nyingine,” alisema rais huyo.

“Kwa hiyo, kama Pierre akisaini mkataba na timu yenye shauku, atakuwa amepata sehemu sahihi. Ukimtazama binafsi, sote tunakubali kwamba ni mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani. Lakini ushauri ninaompa ni kuendelea kupambana na kuzivutia timu kubwa zaidi na zenye shauku zaidi.”

 

Mounguengui hayupo pekee katika maoni yake, gwiji wa Arsenal, Ian Wright naye hivi karibuni alikiri kuwa Aubameyang anaweza kuzichezea timu za juu zaidi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad