Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya chama ha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ameshangazwa na kitendo cha mamlaka ya usalama wa anga nchini kutangaza kuvunja safari zote za ndege za kimataifa nchini
Lema ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter akidai kuwa kitendo hicho ni cha kushangaa kwani Dunia kote ndege zilisha zuiliwa kutoka isipokuwa nchini tu
“Eti Tanzania yafuta safari za nje!!nje gani hiyo?takribani Dunia nzima viwanja vya ndege vimefungwa,nyie mlikuwa mnaenda wapi?au MWANZA,KIA,CHATO,JNIA ndio huku mnaita nje?Dunia ina shangaa tunavyo treat hii PANDEMIC.Hata hivyo imendikwa (Baada ya kiburi ni anguko)” ameandika Lema
Taarifa ya kufutwa kwa safari za ndege za kimataifa kuingia nchini inakuja siku chache nara baada ya Rais Magufuli kusema Tanzania haitofunga mipaka kutokana na ugonjwa wa Covid19
Eti Tanzania yafuta safari za nje!!nje gani hiyo?takribani Dunia nzima viwanja vya ndege vimefungwa,nyie mlikuwa mnaenda wapi?au MWANZA,KIA,CHATO,JNIA ndio huku mnaita nje?Dunia ina shangaa tunavyo treat hii PANDEMIC.Hata hivyo imendikwa "Baada ya kiburi ni anguko".— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) April 12, 2020
Lema ni 'nyie' au 'sisi'? Kwani wewe si mtanzania? Kama si mtz basi iache tz alone. Kama ni mtz mbona unajitenga na kuanzisha kejeli kt kipindi hiki ambacho umoja wetu ni muhimu sana kuliko ilivyokuwa awali
ReplyDeleteHuyu Dogo, Mwwachie kama Alivyo,
DeleteHajijui wa Hajitambui.
Tumuombee Mungu, kwa Muda uliobakia.
Inasikitisha Alivyo changayikiwa
Na Kiwewe juu. Sigala Mbaya.