UEFA imeipiga faini Man City kisa ukubwa wa logo ya mdhamini


Shirikisho la soka Ulaya UEFA limeipiga faini club ya Man City ya England kiasi cha Euro 3000 (Tsh milioni 7.6) kwa kosa la kuvaa jezi za mazoezi zinazokiuka sheria.

Kosa la Man City walitenda mwezi uliopita katika mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Real Madrid, Man City wakati wa warm up kabla ya mchezo jezi zao za warm up walizovaa logo ya mdhamini iliyokuwepo ilikuwa kubwa zaidi na kukiuka sheria za mashindano.



Kwa kawaida kuna kiwango cha ukubwa wa Logo inayotakiwa kukaa kwenye jezi lakini Man City waliweka kubwa, UEFA wamewapa Man City siku 90 za kukata rufaa kama wataona wameonewa, mchezo huo wa 16 bora ulimalizika Man City ikishinda 2-1.

Sheria za UEFA zinaeleza kuwa ukubwa wa logo ya mdhamini katika makoti/jezi ya warm up kabla ya mechi au makoti wanayoingia nayo dakika chache kabla ya mchezo kuanza yanapaswa kuwa na saizi ya 20cm square na 200cm square kwa sare zingine zisizokuwa za kuchezea
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad