Haiwezekani Nataka Kupima DNA Nimestuka!! Wanangu Hawajafanana na Mimi


Mwenzenu jamani nahisi nmechakachuliwa,nina mke wangu tumezaa watoto wawili mmoja yuko na miaka mitano na wa pili miwili,kati yetu mimi na mke wangu nahisi kuna kitu kinaendelea na nimefanya uchunguzi wa kina na kuishia kwa majibu ambayo hayaniingii aklini na pili vilevile hawa watoto wanafanana exactly na watu ninao wahisi
Nkijaribu kurudisha hisia nyuma naona matukio yanafanana na mke wangu pia alikuwa amejipatia ujauzito kwenye mazingira ya kutatanisha,Huyu wa kwanza anafanana sana na boyfriend wake wa zamani ambaye mimi namjua!kipindi yuko mjamzito nilishawahi kumfuma na meseji kibao za mahapa na njemba hilo!
Huyu wa pili anafanana sana na Babu mmoja hapa mtaani kwetu anashona viatu
Huyu mara nyingi nmeshawahi kumkuta home anajisingizie kuja kuchukua viatu,mbaya zaidi hata huyu mtoto huyu mwwanamke anajitahidi sana kumjengea mazoea nae
Sasa naombeni ushauri jamani mm nifanye nini?
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole ndugu yangu, kutokana na wasiwasi huo ulio nao ni bora ukapime DNA ili uwe na uhakika kuwa watoto unaowalea ni damu yako kweli maana hakuna kitu kibaya kulea watoto ambao siyo damu yako, kumbe baba zao wapo wanakuchora tu, hiyo ni haki yako ya msingi, unajua wanawake siku hizi wengi si waaminifu hivyo kubambikiwa mimba isiyo yako ni rahisi sana, unamuoa mwanamke ambaye tayari yupo kwenye mahusiano na wanaume wengine tena si mwanaume mmoja ni wengi.kama umeyapata maoni yangu naomba unijibu ili nijue ujumbe umekufikia.

    ReplyDelete
  2. Pole sana ndugu yangu, ni bora ukapime DNA ili upate uhakika kama watoto ni damu yako kweli au umebambikiwa, kama umeupata ujumbe wangu naomba unijibu haraka sana.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad