Hali Yazidi Kuwa Tete Marekani Wagonjwa Wafikia 600,000


Kwa mujibu wa taarifa zinazotolewa na chuo kikuu cha John Hopsin nchini Marekani idadi ya wagonjwa wa Corona nchini humo imefika 660,000 mpaka kufikia leo

Idadi hiyo ya wagonjwa inaifany Marekani kuwa nchi kinara wa maambuki kwa sasa ukitoa China ambayo ni kitovu cha ugonjwa huo asilimia 33 ya wagonjwa wakiwa kwenye ngi hiyo

Kwa masaa 24 yakiyopita Marekani iliripoti jumla ya wagonjwa wapya takribani 30,000 na vifo visivyopungua 2,000 huku dunia nzima kukiwa na wagonjwa Milioni 2 na vifo 145,000 na watu 547,000 waliripotiwa kupona

Katika hatua hiyo basi mamlaka ya chakula na dawa nchini humo FDA imesema ipo kwenye hatua za mwisho za kutoa vifaa vya kupima virusi hivyo nyumbani ambavyo vitagawiwa kwa wananchi


Ikumbukwe kuwa Marekani ni moja kati ya nchi nyingi duniani iliyozuia wananchi wake kutoka nje
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad