Hamisa Mobetto Kama Faith EVANS Alivyowachezea TUPAC na BIG..Acheza Pande Zote Mbili WCB na KINGS Music..Ataweza Kweli?



FAITH Evans alikuwa mke wa Rapa Notorious BIG ambaye alitambulika kuwa hasimu wa Tupac Shakur.

Hamisa Mobetto alikuwa mpenzi na aliishi kinyumba na Diamond Platnumz ambaye inafahamika ni hasimu wa Alikiba.

Faith katika ndoa yake na BIG, amepata mtoto mmoja, CJ Wallace.

Hamisa katika mapenzi yake na Diamond, amepata mtoto mmoja.

Faith alikuwa mwanamuziki chini ya lebo ya Bad Boy Entertainment iliyokuwa na uhasimu na Death Row Records.

Hamisa ni mwanamuziki pia, japo hajasainiwa WCB, ameshafanya kazi kama model kwenye wimbo "Maria Salome" wa Diamond ft Rayvanny, WCB, lebo yenye upinzani na Kings Music.

Desemba 1995, Faith akitambua Tupac ni hasimu wa BIG (mumewe), alikubali mwaliko wa kuimba chorus ya wimbo "Wonda Why They Call You Bitch" wa Tupac. Tena, kazi ilifanyika studio za Death Row Records ambayo haiivi na lebo yake ya Bad Boy.

Aprili 2020, Hamisa ametokea kwenye video ya wimbo "Dodo" wa Alikiba. Wimbo umefanywa Kings Music Records, yenye upinzani na WCB ya mzazi mwenzake, Diamond.

Baada ya kukamilisha recording session ya "Wonda Why They Call You Bitch", Tupac aliachia mkwaju wa ugomvi "Hit Em Up", akimsiliba BIG kuwa yeye (Tupac) alitembea na mkewe, Faith.

Inadaiwa Faith alikwenda Death Row kufanya wimbo na Tupac, kumlipizia BIG aliyekuwa akisaliti sana nje ya ndoa na marapa wa kike, Lil Kim na Charli Baltimore. Vilevile BIG alimdiss Faith kwenye wimbo "Get Money" ft Lil Kim, halafu Charli yupo kideoni.

Hamisa 'aliitwaga' mchawi eeh? Mchafu sio? Ndio naye analipiza? Au yeye na Ali ni kikazi zaidi.

Faith kupitia kitabu chake "Keep The Faith" kilichotoka mwaka 2008, anakiri kila alichofanya na Tupac hakikuwa sawa.

Faith ameandika kuwa alipomaliza kuingiza sauti, Death Row, aliambiwa afuate malipo yake (dola 25,000) kwa Tupac, chumbani, hotelini. Akaenda. Kisha, kule chumbani, Tupac alimlazimisha mapenzi.

Unamfuataje chumbani adui wa mumeo?

Zile taarifa za Hamisa kuwa hotelini na Ali, Zenji, bila shaka ni kikazi tu. By the way, Hamisa sio Faith.

Sema BIG alikuwa player halafu kauzu. Faith alimuuliza "nimesikia unatembea na Lil Kim" akajibu "Yeah, nipo naye mwaka na nusu sasa." Faith hoi!

Ndimi Luqman MALOTO

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad