Harmonize Kuimba Taarabu, Atembelea Kiki ya Mzee Yusuph Kurudi Kwenye Mziki


Staa wa muziki nchini, Harmonize amefunguka na kusema yuko mbioni kuachia wimbo wa taarab na atamshirikisha Mzee Yusuph pindi atakaporudi mjini.

Hivi karibuni aliyekuwa Mwimbaji nguli wa muziki wa Taarab nchini, Mfalme Mzee Yusuph aliweka wazi anatarajia kurejea kwenye muziki ila watu wangoje ni kitu gani hasa atakuja kuimba.

Harmonize akiwa kwenye kipindi cha Uhondo, E FM Radio aliimba kionjo cha wimbo huo ambao kwa sasa anauandaa.

Itakumbukwa, Mzee Yusuph ana miaka takribani 6 tangu alipotangaza kuachana na muziki huo na kuanza kuimba Qaswida zenye maudhui ya dini ya kiislam. Je akirudi mjini atakuja na maadhi gani ya muziki? Mimi na wewe hatujui, tufanye kusubiri.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii itakuwa umelamba Dume..KondeBoy!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad