Hatujasitisha Kufungisha ndoa, Tumezuia Wanaotaka Kufanya Sherehe - Kanisa Katoriki


Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anaitwa Padri Dr. Charles Kitima amefafanua tamko la Kanisa Katoliki kuzuia watu kufunga ndoa nakusema hawajazuia sakramenti hiyo ila wamezuia wale wanaotaka kufanya sherehe.

“Ibada ya kupokea Sakrament ya ndoa na kipaimara hizi shughuli zisiandamane na shamrashamra, ukishafunga ndoa kusiwepo sherehe, kinachofanyika ni mkusanyiko wa Ibada, kama unataka na sherehe subirisha” Katibu Mkuu TEC

“Ndoa zinaendelea kufungwa, mtu amekaribia kufa huwezi mnyima Ubatizo, nyie Wachumba mmepanga kufunga ndoa April njooni Kanisani mtafunga mko wawili na wasimamizi wanne, distance mita moja moja lakini hamna sherehe” Katibu Mkuu TEC Padri Kitima

“Tafsiri iliyotolewa na baadhi ya Vyombo vya Habari haikuwa sahihi, Askofu hakuwa na maana kwamba anasimamisha sakrament, hakuna anayeweza kusimamisha huduma za Yesu” Katibu Mkuu TEC Padri Kitima

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad