Hii Hapa Idadi ya Watu Waliopona Baada ya Kupata Ugonjwa wa Corona


TAKWIMU mpya za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zinaonyesha kuwa, watu 3,235 waliokuwa wameambukizwa virusi vya corona katika nchi 52 za Afrika wamepata afueni.

Takwimu hizo zilizotolewa mapema jana (Aprili 15) zinasema kuwa, kesi 16,265 za wagonjwa wa Covid-19 zimethibitishwa kufikia sasa katika nchi hizo za Afrika.

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, watu 873 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona barani Afrika.

Nchi 52 za Afrika zimeathiriwa na virusi vya corona huku nchi mbili za Lesotho na Comoro zikiwa hazina kesi yoyote hadi sasa ya ugonjwa huo angamizi wa kuambukiza.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Algeria inaongoza kwa idadi ya vifo na maambukizo barani Afrika na kwamba hadi sasa, watu zaidi ya 300 wamekufa kwa corona katika nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika na walioambukizwa ni karibu 2,000.

Marekani inaongoza kwa maambukizo na vifo vya corona duniani, ambapo hadi jana mchana watu 2,228 waliaga dunia na kusababisha idadi ya walipoteza maisha kwa ugonjwa huo hadi sasa katika nchi hiyo kufikia 28,300.

Waliokufa kwa Corona kote duniani hadi sasa ni zaidi ya 120,000 huku idadi ya walioambukizwa virusi hivyo ikikaribia milioni 2.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad