Hospitali Yatoa Maagizo, Barakoa Zilizotumika

 

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando iliyopo mkoani Mwanza, imeagiza kuwa mtu yeyote, awe mgonjwa ama ndugu wa mgonjwa atakayefika kwenye Hospitali hiyo atagawiwa Barakoa getini na kwamba atatakiwa kuirejesha getini kabla hajatoka.

Taarifa hiyo imetolewa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ya hospitali hiyo, na kwamba kuanzia leo Aprili 24, 2020, kila mtu atakayefika hospitalini hapo atapaswa kuvaa Barakoa, ikiwa ni tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona.

"Katika kuendelea kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona, uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando unawafahamisha umma kwamba kuanzia Aprili 24, yeyote atakayefika hapa atatakiwa kuvaa Barakoa, hivyo kila mmoja atapewa Barakoa getini na atatakiwa kuirudisha kabla hajatoka getini" imeeleza taarifa hiyo.

Mpaka sasa Tanzania imekwisharipoti visa 284 vya watu waliopata maambukizi ya Virusi vya Corona, na 256 kati yao wanaendelea vizuri, 7 wakiwa katika uangalizi maalum kutokana na hali zao za kiafya, huku vifo navyo vikiwa ni 10, na leo Aprili 24, 2020, pia Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, ametangaza kuwa jumla ya wagonjwa 37 wa Virusi vya Corona wamepona na wameruhusiwa kurejea makwao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad