Serikali imetangaza kwamba wasafiri wote kutoka Nchi zilizoathirika na corona watalazimika kukaa karantini kwa siku 14 katika hosteli za UDSM maarufu ‘hosteli za Magufuli’ na utaratibu wa Mahoteli hautokuwepo tena, kwa lengo la kudhibiti mienendo yao saa 24.
“Tumeona kule Iringa, kuna wasafiri tuliwaweka hotelini wakatoroka, ili kudhibiti mienendo ya wasafiri na kuwalinda Watanzania wengi tumeona tuwaweke sehemu moja (hosteli za Magufuli) ambako kutakuwa na ulinzi saa 24, RC Makonda atasimamia kwa karibu chini ya Wizara ya Afya”-Waziri wa Afya Ummy Mwalimu