Huenda binti wa Mayweather akahukumiwa miaka 99 jela kwa kosa la kumchoma kisu mara mbili mwanamke aliyezaa na mchumba wake Youngboy



Taarifa zilizosambaa siku ya leo kutoka nchini Marekani ni hizi zinazomhusu binti wa Floyd Mayweather, Iyanna (20) huwenda akahukumiwa kifungo cha hadi miaka 99 jela kwa kosa la kumchoma Kisu mara mbili baby mama wa NBA Youngboy. (Mwanamke aliyezaa naye)

Tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita (April 4) ambapo mkasa ulianza baada ya Iyanna kuwasili nyumbani kwa mpenzi wake, rapper NBA YoungBoy ambapo alimkuta na baby mama wake huyo aitwaye Lapattra Lashai Jacobs. Iyanna alianza kumwambia Lapattra aondoke hapo nyumbani kwani NBA Youngboy ni mchumba wake.

Baada ya kuzozana sana walifikishana hadi jikoni ambapo binti huyo wa Floyd alichukua visu viwili, pale Lapattra alipozidisha hatua tu, Iyanna alimchoma kisu kimoja.

Akiwaambia polisi, Lapattra alisema hakusikia kisu cha kwanza kilivyoingia, na Iyanna alimshindilia tena kisu cha pili.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast, Iyanna alishtakiwa kwa kosa la kushambulia mtu na silaha ya hatari, kosa la jinai ambalo linabeba faini ya ($10K) TSH. Milioni 22 au Kifungo cha miaka 99 Jela. Kwa sasa yuko nje kwa dhamana ya TSH. Milioni 68.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad