Watu 12 wamegundulika kuwa na virusi hivyo vya corona nchini Kenya katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Idadi ya waliokufa kutokana na virusi hivyo pia imeongezeka hadi wanne baada ya mtoto wa miaka sita kufariki.
Mtoto wa miaka sita amefariki dunia kutokana na virusi vya corona nchini Kenya na kufikisha idadi ya watu walioaga dunia kutokana na ugonjwa huo kuwa wanne, huku watu walioambukizwa ugonjwa huo ikifikia 122. Hayo ni kwa mujibu wa wizara ya Afya. Wakati huo huo, taifa hilo la Afrika Mashariki limeanza kujitengenezea barakoa zake.
Katika kipindi cha saa 24 zilizopita watu 12 wamegundulika kuwa virusi hivyo vya corona nchini Kenya. Akizungumza na wanahabari waziri msaidizi katika wizara ya Afya Mercy Mwangangi amesema kati ya visa hivyo vipya vilivyotangazwa leo, watu 11 ni raia wa kenya na raia moja wa Somalia. Kati yao, wagonjwa wanane ni wa kiume huku wanne wakiwa wanawake. Watu walioambukizwa ugonjwa huo hadi kufikia sasa ni watu wenye umri wa miaka 28 hadi 68. Watu hao 12 wamewekwa kwenye karantini mbali mbali za taifa.
Hadi kufika sasa watu 1,433 wamewekwa kwenye karantini huku wengine 617 wakitarajiwa kutengwa. Wakati huo huo serikali imeanza kutengeneza barakao ambazo zitasambazwa kupitia kwa serikali za majimbo kwa bei nafuu.
Serikali ya Kenya imesema itawaajiri wahudumu wa afya 5000 zaidi katika siku chache zijazo kuimarisha vita dhidi ya corona
Serikali ya Kenya imesema itawaajiri wahudumu wa afya 5000 zaidi katika siku chache zijazo kuimarisha vita dhidi ya corona
Serikali imesema viwanda ambavyo vinatengeza barakao hizo vina uwezo wa kutengeza barakao milioni 60. Washonaji wa chereheni pia wataruhusiwa kutengeza barakao hizo. Alhamisi serikali ilitangaza visa vipya 29, idadi kubwa zaidi kuwahi kutangazwa tangu maradhi hayo yalipobisha hodi nchini. Betty Maina ni wziri wa biashara na Viwanda.
Ili kuimarisha vita dhidi ya ugonjwa huo serikali imetangaza kuwa itaawajiri Wahudumu 5000 wa afya katika kipindi cha siku saba zijazo katika majimbo yote 47. wataajiriwa kusaidia kukabiliana na maambukizi ya covid-19 katika majimbo. Wahudumu hao wanakabiliwa na hatari wanapowauguza wagonjwa suala ambalo Katibu wa Muungana wa vyama vya wauguzi nchini Seth Panyako anasema linastahili kuangaziwa na serikali.