Imeelezwa jinsi taifa la Korea Kusini lilivyofanikiwa kuzuia maambukizi ya corona


Virusi vya corona vilitambuliwa rasmi kama janga. China, Italia, Iran na Korea Kusini hadi kufikia leo ni miongoni mwa mataifa yaliyoathirika zaidi ya usambazaji wa virusi vya corona, na serikali zao zimechukua hatua kukabiliana na usambaaji wa virusi hivyo.

China ilitenga miji na kujenga hospitali chini ya wiki moja kukabiliana na hali hiyo ya dharura huku serikali ya Italia ikitangaza hatua za kujitenga katika eneo zima la rasi hiyo.

Lakini kuna kisa kimoja ambacho kinachukuliwa kama mfano wa kuigwa: Korea Kusini.

Licha ya kwamba idadi kubwa ya watu waligunduliwa na virusi vya corona, idadi ya vifo ilikuwa asilimia 0.6 chini zaidi ikilinganishwa na Marekani, Italia na Iran.

Ramani inayoonesha usambaaji wa virusi vya Corona: Kote Duniani hadi kufikia Aprili 6, 2020

Je, Korea Kusini imefanikiwa vipi kukabiliana na virusi vya corona na je nchi zingine zinaweza kujifunza nini?

“Korea Kusini ilifanya kampeni makhususi ya kupambana na virusi vya corona. Serikali ilitangaza kwamba vituo vyote vya afya vianze kupima ugonjwa wa Covid-19 nyakati za mwanzo mwanzo katika maeneo yaliyoathirika zaidi,” anaelezea Bugyeong Jung, mwanahabari wa BBC kitengo cha Korea Kusini.

Mfano wa hili ni kwamba licha ya kuwa Marekani na Korea Kusini zote zilitangaza visa vya kwanza vya corona siku moja, (Januari 20), hadi wiki hii ilikuwa imepima watu 4,300 katika eneo lake.

Korea Kusini, upande wake, ilipima watu 196,000.

“Ingawa njia hii wengi wanasema ni kama uvamizi, imefanikiwa kuokoa maisha ya watu wengi,” ameongeza Jung.

Halaiki ya watu kupimwa kwa wakati mmoja
Janga hilo lilipotokea, mwishoni mwa 2019 kaskazini mwa China, wengi wangetabiri kwamba mataifa jirani ndio yangekuwa ya kwanza kuathirika.

Januari 20, Korea Kusini ilithibitisha kisa chake cha kwanza cha virusi vya corona.

Punde tu, mfumo wa afya wa Korea Kusini ukabaini kitovu cha janga hilo nchini humo: Mji wa Daegu, eneo la kaskazini, ambapo robo tatu ya visa vyote vya ugonjwa wa covid-19 vilithibitishwa nchini humo.

Na kati ya visa hivyo, asilimia 63 ya maambukizi yalikuwa yanahusishwa na kundi la kidini kama la Church of Jesus huko Shinchonji, dhehebu ambalo linaendeleza kazi ya Lee Man-hee, mwanzilishi wake.

“Korea Kusini imekuwa ikijitayarisha kukabiliana na janga hili tangu mwaka jana, wakati ilipokumbwa na ugonjwa wa MERS (ugonjwa wa matatizo ya kupumua uliosambaa sana nchi za Mashariki ya Kati),” anasema Jung.

Daegu ni mji wa Korea Kusini ambapo mlipuko huo ulianzia miongoni mwa mataifa ya bara Asia
Daegu ni mji wa Korea Kusini ambapo mlipuko huo ulianzia miongoni mwa mataifa ya bara Asia
Mkakati huo ulioratibiwa na Wizara ya Afya ya Korea Kusini, ulianzishwa kuanzia siku ya kwanza: ukiwa ni mtandao makhususi wa kupima virusi hivyo ukilenga kupunguza idadi ya vifo.

“Kubaini virusi hivyo mapema ni muhimu ili kuweza kugundua walioathirika na virusi hivyo na hilo litawezesha kuzuia kusambaa ama kupunguza kasi ya usambaaji,” Park Neunghoo, Waziri wa afya wa Korea Kusini amezungumza na shirika la CNN.

“Hili pia limewezesha kuwa na mipango mizuri katika mfumo wa Afya, kwasababu asilimia 10 tu ya waliokuwa wameambukizwa walihitaji kuwa hospitali, ” aliongeza.

Kwa wataalamu, mbinu iliyotumiwa na Korea Kusini ndio yenye kuchangia matokeo bora zaidi kwasababu inawezesha kuona kiuhalisia kile kinachoendelea.

“Korea Kusini imekuwa ikifuatilia watu 10,000 kwa siku, wengi wao wakiwa ni wale waliothibitishwa kuwa na virusi hivyo na walionesha dalili za wastani,” Profesa wa chuo kikuu cha Hong Kong mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza Benjamin Cowling ameiambia BBC World .

China, Italia, Iran na Korea Kusini hadi kufikia leo ni miongoni mwa mataifa yaliyoathirika zaidi ya usambaaji wa virusi vya corona, na serikali zao zimechukua hatua kukabiliana na usambaaji wa virusi hivyo.

China ilitenga miji na kujenga hospitali chini ya wiki moja kukabiliana na hali hiyo ya dharura huku serikali ya Italia ikitangaza hatua za kujitenga katika eneo zima la rasi hiyo

Lakini kuna kisa kimoja ambacho kinachukuliwa kama mfano wa kuigwa: Korea Kusini.

Licha ya kwamba idadi kubwa ya watu waligunduliwa na virusi vya corona idadi ya vifo ilikuwa asilimia 0.6 chini zaidi ikilinganishwa na Marekani, Italia na Iran.

Ramani inayoonesha usambaaji wa virusi vya Corona: Kote Duniani hadi kufikia Aprili 6, 2020

Je Korea Kusini imefanikiwa vipi kukabiliana na virusi vya corona na je nchi zingine zinaweza kujifunza nini?

“Korea Kusini ilifanya kampeni makhususi ya kupambana na virusi vya corona. Serikali ilitangaza kwamba vituo vyote vya afya vianze kupima ugonwa wa covid-19 nyakati za mwanzo mwanzo katika maeneo yaliyoathirika zaidi,” anaelezea Bugyeong Jung, mwanahabari wa BBC kitengo cha Korea Kusini.

Mfano wa hili ni kwamba licha ya kuwa Marekani na Korea Kusini zote zilitangaza visa vya kwanza vya corona siku moja, (Januari 20), hadi wiki hii ilikuwa imepima watu 4,300 katika eneo lake.

Korea Kusini, upande wake, ilipima watu 196,000.

“Ingawa njia hii wengi wanasema ni kama uvamizi, imefanikiwa kuokoa maisha ya watu wengi,” ameongeza Jung.

Wakosoaji
Lakini mkakati huo pia umekosolea.

Mwanahabari wa BBC Hyung Eun Kim anasema inasemekana kwamba taarifa ambazo serikali imejua na inasambaza ni pamoja na jirani yako aliyepata virusi vya corona ambako kumepata upinzani mkali.

Mbali na vipimo vingi ili kuwagundua walioambukizwa , kuna muda wa kuosha treni, subway na mabasi
Mbali na vipimo vingi ili kuwagundua walioambukizwa , kuna muda wa kuosha treni, subway na mabasi
“Kuna hofu ambayo imejengwa kati ya watu wa miji mbalimbali. Kila wakati watu wanapokea taarifa kuhusu watu walioambukizwa katika simu zao,” anasema mwanahabari huyo.

“Hilo limesababisha wengi kuomba serikali kutoweka wazi taarifa zao binafsi, kwasababu ya athari ambazo zinaweza kutokea baada ya hapo,” aliongeza.

Mkakati huo unaonekana kufanikiwa kwa kuzingatia idadi ya wanaoambukizwa katika kipindi cha siku 11, ambacho kimefanya serikali kufikiria kwamba tayari janga hilo limeshafikia kilele chake na kwamba sasa hali ilivyo ni kuwa umeanza kudhibitiwa.

Hatahivyo, Jumatano, waziri mwenywe alitangaza kubainika kwa visa 90 ambavyo, na hilo linaongeza tena idadi ya walioambukizwa nchini humo.

Sababu kuu ilikuwa ni kugundua maambukizi kupitia kituo kimoja kilichopo mji mkuu wa Seoul.

“Maambukizi hayo katika kituo hicho huenda ikawa ni wimbi jipya la maambukizi na pengine linaweza kusababisha mlipuko na kusambaa tena kwa janga hilo,” Park amesema hivyo katika taarifa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad