JESHI la walinzi wa kimapinduzi nchini Iran limesema limepeleka setalaiti yake ya kwanza ya kijeshi katika mzunguko wa dunia.
Wataalamu wamesema Iran imezindua kile walichokiita mpango wa siri wa safari za anga za juu ambao unaanza wakati kukiweko mivutano baina ya nchi hiyo na Marekani.
Hata hivyo, hakuna taarifa iliyotolewa mara moja na chombo huru kuthibitisha kurushwa kwa setalaiti hiyo ambayo jeshi la ulinzi wa kimapinduzi limeiita ‘Nuru”.
Wizara ya mambo ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ambayo imekuwa ikisisitiza kwamba hatua kama hiyo ya kurusha setalaiti inaisogeza mbele Iran katika mpango wake wa kutengeneza makombora ya masafa marefu, haijatoa taarifa yoyote.
OPEN IN BROWSER