Iran yasema kamwe haitoiomba Marekani Msaada wa Kupambana na Corona



Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Abbas Moussavi amesema Iran kamwe haitoitisha msaada kutoka kwa Marekani katika mapambano dhidi ya virusi vya corona.

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amekataa ombi la Marekani la msaada wa kiutu wakati ambapo Iran ndiyo nchi iliyoathirika zaidi Mashariki ya kati ikiwa na zaidi ya watu elfu tatu mia sita walioaga dunia na karibu sitini elfu walioambukizwa.

Kumekuwa na mivutano mikubwa kati ya nchi hizo mbili tangu mwaka 2018 pale Rais Donald Trump alipoiondoa Marekani kutoka kwenye mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 ulioiondolea vikwazo Iran.

Baada ya tukio hilo Marekani iliiwekea Iran vikwazo vipya ambavyo vimeulemaza uchumi wa nchi hiyo.

Uongozi wa Iran unasema vikwazo vya Marekani vinaifanya nchi hiyo kutokuwa katika nafasi nzuri ya kupambana na virusi vya corona na kuzitaka nchi zingine pamoja na Umoja wa Mataifa kuitaka Marekani iviondoe vikwazo hivyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad