“Namuomba Rais Kenyatta achukue hatua ambazo Museveni amechukua, Museveni amepiga marufuku wapangaji kutimuliwa na Maboss kisa hawajalipa kodi, Wakenya wengi hawaendi kazini kisa corona, hawana pesa, Serikali izuie pia Mabenki kudai wamiliki wa nyumba wenye madeni”-Charles Kangi Jaguar Mbunge wa Starehe
“Wapangaji kutimuliwa kisa kodi wakati tunakabiliwa na corona, ni hatari kwa afya na itatugharimu, watawezaje kutekeleza agizo la kutotembea usiku wakiwa wanapigwa baridi mtaani, wengine watafanya uhalifu ili watunze Familia zao, tuzuie wenye nyumba wasiwatimue wapangaji” -JAGUAR
“Wamiliki watakaoweza kuwasamehe kabisa kodi wapangaji wafanye hivyo kama Rais Kenyatta alivyoshauri, wengine watakusanya kodi zao janga la corona likiisha, wapangaji wanaoweza kulipa yote au nusu walipe, wasioweza wasitimuliwe kwenye nyumba, pesa ni ngumu muda huu”-JAGUAR