Jamaa Aeleza Kuhusu Dawa Aliyoitumia Kumtibu Nduguye Aliyepatikana na Corona
0
April 13, 2020
Bwana mmoja ameiwasha mitandao ya kijamii baada ya kudai kuwa alimtibu kikamilifu nduguyu ambaye alipatikana na virusi vya corona.
Kulingana na video yake iliyosambaa mitandaoni, jamaa huyo anaeleza kuwa nduguye alifanyiwa vipimo na kupatikana na virusi hivyo baada ya kuanza kuonyesha dalili za maradhi hayo.
Alionyesha tangawizi, kitunguu saumu maji moto na viungo vingine alivyodai kuwa ndivyo alivyovichanganya na kutumia katika kumtibu nduguye aliyekuwa akiugua.
Katika video hiyo, alisimulia jinsi ya kuandaa dawa hiyo ambayo alimnywesha nduguye kila baada ya masaa manne.
Kulingana naye, baada ya siku tatu tu, virusi vya corona viliisha na nduguye kupona kikamilifu kutokana na maradhi hayo.
Alieleza kuwa hakutaka kutangaza kuhusi jinsi alivyomtibu nduguye kwa dawa hizo za kienyeji lakini akasukumwa na kulazimika kubaini wazi.
Jamaa huu amedai kuwa nduguye aliyepona alimlazimu kuichapisha video hiyo mtandaoni ili kuweza kuwasaidia wengine katika kupambana na virusi hivyo.
Virusi vya Corona vimekuwa tishio kubwa si kwa Tanzania tu bali kwa ulimwengu mzima, uchumi ukizoroteka na wengi kukosa nafasi za ajira kwavyo.
Hadi sasa idadi maambukizi ya virusi hivyo vya corona vimefika 32, vifo 3 na watu watano kupona kutokana navyo.
Hayo yakijiri, Rais Magufuli ametangaza kupiga marufu usafiri wa ndege za kimatafa nchini kama njia ya kudhibiti virusi hivyo.
Tags