Jamii Yatakiwa Kuacha Kufumbia Macho Ukatili Watoto Ufanywao na Ndugu Kweye Familia



Na Baraka Messa, Songwe
JAMII yatakiwa kuacha kufumbia macho ukatili wa watoto unaofanywa na ndugu ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo bado vinaendelea katika baadhi ya maeneo mkoani Songwe.

Hayo yalibainishwa na Mkaguzi msaidizi  wa jeshi la polisi kutoka dawati la jinsia na watoto Mkoa wa Songwe Debora Mhekwa alipozungumza na gazeti hili hivi karibuni, ambapo alisema matukio yaliyo mengi hufichwa kutokana na kufanywa ndugu katika familia hivyo familia kuogopa kuchukua hatua muhimu kwa kuhofia kumuumiza ndugu aliyehusika.

  Mhekwa alifafanua kuwa asilimia 90 ya watoto wanaofanyiwa ukatili takwimu zinaonyesha kuwa vitendo hivyo hufanyika ndani ya familia , hivo kuitaka jamii kutofumbia matukio hayo kwa kuwa huhatarisha maisha ya watoto ambapo anadai kuwa wahanga wakubwa ni kuanzia umri wa miaka mitano na kuendelea.

"Matukio kama ubakaji, ulawiti watoto kutoroshwa watoto mara nyingi hufanyika ndani ya familia na ndugu, wazazi na jamii waache kufumbia changamoto hizi amabazo ni hatari kwa mtoto, tuwe karibu na tuwe marafiki wa watoto ili watoto wawe huru kutueleza changamoto wanazokumbana nazo wakiwa shuleni na nyumbani" alisema Mhekwa.

Alisema jeshi la polisi kupitia Dawati la jinsia na watoto wamekuwa wakitoa elimu kwa wanafunzi mashuleni, kuandaa midaharo mbalmbali na kuandaa mikutano ya hadhara vijijini kwa kila wilaya wakiwa na lengo la kuelimisha jamii kuachana na matukio ya unyanyasaji watoto na umuhimu wa kuwa karibu na watoto ikiwa ni pamoja na kutoa mahitaji muhumu kwao.

"Kupitia elimu hiyo pia wananchi wanapata fulsa ya kujua pia sheria mbalimbali kwa mfano tunawaelimisha kuwa mtu akibaka au kulawiti "adhabu yake ni miaka 30 jela kwa mujibu wa sheria ya adhabu", mpaka sasa matukio yamekuwa yakipungua kila mwaka japo kuwa kuna changamoto kwa baadhi ya jamii kulindana kutokana na matukio mengi kuwa ndani ya familia" alisema Mhekwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Songwe Lucia Manongi alisema wazazi walio wengi wamekuwa wakishindwa kukaa na watoto wao kwa kusingizia kuwa wanatingwa na shughuli mbalimbali za kiuchumi huku wakiwaacha watoto wakijifanyia vitu vingi bila kuongozwa hali ambayo ni hatari katika malezi na makuzi ya awali ya mtoto.

Alisema mzazi ndio mwalimu wa kwanza kumfundisha ,kumlea na kumlinda mtoto ,hivyo kuwataka wazazi kubadilika na kuwa karibu na watoto muda mwingi ili kujua mienendo na tabia za watoto tangia wakiwa na umri wa chini ya miaka mitano.

''Tusiwaachie walimu pekee katika ulinzi wa watoto, tutoe pia ushirikiano kwa wale wote wanaohusika na ukatili wa watoto bila kujali undugu uliopo katika familia na mhalifu" aliongeza Manongi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad