Jaribio la Kwanza la Dawa ya Kuzuia Corona Kufanyiwa Nchini Kenya – Wanasayansi Kutoka Uingereza wasema
0
April 24, 2020
Ni jambo ambalo huenda litawashangaza wengi, lakini swali linalosalia katika akili za watu ni je, ni nani aliyependekeza hatua hiyo ya kufanyia jaribio hilo katika taifa la Kenya?.
Wanasayansi kutoka Uingereza wamesema kuwa watafanyia majaribio ya dawa ya kuzuia virusi vya Corona katika taifa la Kenya kwa kile wamesema huenda idadi ya maambukizi nchini ikaongezeka.
Wanasayansi hao kutoka chuo kikuu cha Oxford wanatazamia kuchukua hatua hiyo iwapo hawatapata matokea kamili kwa ambao wanawafanyia vipimo kule Uingereza.
Fergus Walsh akiwa kwa mahojiano na shirika la BBC alisema iwapo majaribio yanayoendelea kufanyika katika taifa la Uingereza yatafeli basi wataangazia kusafiri hadi nchini Kenya ili kubaini iwapo dawa hiyo inafanya kazi.
Ukoloni Mamboleo! Watanzania 2 watupwa baharini na Wachina kwa hofu ya kuwaambukiza Corona
Kulingana na Walsh, chuo cha Oxford kina rekodi nzuri ya kutengeneza dawa za kuzuia dhidi ya virusi hatari ikiwa ni zaidi ya miaka 30 .
Tags