JE Corona Imetengenezwa Maabara?



Daktari wa Ufaransa aliyeshinda tuzo ya Noble Medicine award mwaka 2008 Luc Montagnier amesema kuwa virusi vya Corona(Covid-19) vilitengenezwa katika maabara huko Wuhan, Uchina.

Luc Montagnier ameandika kwenye tovuti ya "daktari wa Pourquoi" kuwa haamini kwamba Covid-19 ilitoka katika soko la wanyama huko Wuhan.

"Covid-19 ilitengenezwa kutoka maabara huko Wuhan. Maabara hii imekuwa ya kitaalamu katika kutengeneza virusi vya corona tangu miaka ya 2000." Montagnier amesisitiza kwamba amekuwa akichunguza suala hili vizuri.

Montagnier amesema katika taarifa yake kwenye kituo cha CNEWS kuwa,

"Virusi hivi havikuanza kwa njia ya kawaida, ni kazi ya kitaalam. Sijui vimetengenezwa kwa nia gani.".

Daktari huyo mtaalamu ameendelea kufafanua na kusema kuwa kuna uwezekano ya kwamba virusi vya Corona vina chembechembe ya virusi vya UKIMWI ndani yake.

"Hii inaweza kuwa ni njia ya kupata chanjo dhidi ya virusi vya UKIMWI" alisema.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad