Kamanda Muroto afunguka sababu za kuzuia mkutano wa Mbowe


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa jana walizuia mkutano wa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kwa lengo la kumlinda yeye pamoja na waandishi, kutopata maambukizi ya Virusi vya Corona na kwamba kama alikuwa na jambo la kuliambia Taifa angeenda kulisemea Bungeni.

Hayo ameyabainisha leo Aprili, 23, 2020 na kusema kuwa kwa sasa Serikali imepiga marufuku mikusanyiko ya watu wengi na kwamba hatua hizo walizichukua kwa lengo la kuwalinda wote kwa pamoja.

"Sababu kubwa alikuwa anafanya mikusanyiko ndani ya ofisi zake, tulikuwa tunainusuru hali yake ya kiafya na waandishi wetu wa habari, kwanza walishatuhumiwa na familia yake kama wana maambukizi na kama alikuwa na jambo la msingi la kuliambia Taifa angeenda Bungeni, mikusanyiko ni marufuku" amesema Kamanda Muroto.

Jana Aprili 22, 2020, Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, alikuwa na mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo jijini Dodoma, lakini baadaye Jeshi la Polisi lilifika kwenye ofisi hizo na kuzuia mkutano huo.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hatua uliyochukua Kamanda ni Sahihi..!!!

    Kolona siyo ya kuchezea.

    Na huyu ndugu yetu ilibidi ajikalantini siku zisizopungua 60. manake Dudley ni mmoja wapo.

    Ruzuku itamfikia hata kwa Tigo pesa. Ni bora Apumzike na kujikalantioni.

    waandishi muwe makini nani mnaokutana Nao.

    Asante Kamanda. Ningeomba Mumuchukue kumpima kolona ili ajiridhishe na kujilinda na Kuilinda Jamii.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad