Kanisa Katoliki Lapiga ‘STOP’ Mafundisho, Kwaya


Ikiwa ni Takribani siku mbili Tangu waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Kasim Majaliwa kutoa muongozo kwa vyombo mbalimbali kuchukua hatua ili kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini baraza la maaskofu wa Kanisa  Katoliki Tanzania ‘TEC’ limetoa tamko ikiwa  sehemu ya utekelezwaji wa agizo hilo

Katika taarifa iliyotolewa kwa Umma TEC imeamua kusitisha mara moja shughuli za mazoezi ya kwaya za kanisa nchini nzima  ili kuepuka mikusanyiko pili TEC Imetangaza kusitisha nyimbo wakati wa ibada ili kufanya misa ziwe za muda mfupi



Mbali na Kwaya  mafundisho ya dini kwa watoto na makundi mengine yamesitishwa na yataendelea kwa njia nyingine kama kujisomea Katekisimu au kwa njia ya mtandao

Lakini Pia kanisa litatoa vifaa vya kujikinga na usambaaji wa virusi hivyo kwa watumishi wa kanisa wanaokaa na watu wanojitaji huduma ya kiroho pia watatakiwa kutoa elimu kwa watu hao juu ya Corona

Wakati wa Ibada TEC imesema Kanisa litazingatia kuwa na umbali kati ya mtu na mtu wanapokuwa Ibadani, matumizi ya vinasa sauti, Waumini kunawa mikono kabla ya kuingia Kanisani na vifaa vya Ibada kunyunyuziwa dawa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad