Kanisa: Sri Lanka Lasamehe Walioua Watu 279

 

Kanisa Katoliki nchini Sri Lanka jana limesema kuwa limewasamehe wote waliofanya shambulizi la kujitoa muhanga ambalo liliua watu 279 wakati wa Pasaka mwaka jana.

Kardinali Malcolm Ranjith alisema katika ibada ya Pasaka iliyorushwa moja kwa moja kutoka kituo cha televisheni kutokana na mlipuko wa virusi vya corona kwamba “tunawapa upendo maadui waliojaribu kutuangamiza”.

“Tunawasamehe,” alisema, akiongeza kuwa badala ya kulipa kisasi, taifa hilo lenye waumini wengi wa Kanisa Katoliki, limetafakari ujumbe wa Yesu wa tumaini na kuondoa taharuki.

Washambuliaji wa tukio hilo la Jumapili ya Aprili 21 mwaka jana walilenga makanisa matatu na hoteli tatu za kifahari, na kuua takriban watu 279 na kujeruhi wengine 593.

Mwaka jana, Ranjith aliitaka serikali wakati huo kujiuzulu kutokana na tuhuma kuwa ilishindwa kuchunguza “njama za kimataifa” zilizokuwa nyuma ya mashambulizi hayo.

Serikali hiyo ya Rais Maithripala Sirisena, ilishindwa katika uchaguzi wa Novemba mwaka jana, huku mdogo wa rais wa zamani, Mahinda Rajapaksa, akishika hatamu.

Washtakiwa kwa mauaji
Awali Sirisena aliwashutumu Waislamu wenye imani kali kuwa walihusika na shambulio hilo, lakini baadaye alilituhumu genge la kimataifa la wauza dawa za kulevya kuwa ndilo lililohusika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad