Kayumba Amjibu Mkubwa Fella Sakata la Utapeli Bongo Star Search 'Hilo Gari Nililonunua Tulienda Wote Show Room?"


Baada ya Risala ya Mkubwa Fella kijana Kayumba akasema silazi damu bwana nakupa za uso hapa hapa. Na yeye akajibu kupitia ukurasa wake wa Instagram akaandika:

BINADAM WATAKUKOSEA, ALAF WATATENGENEZA MAZINGIRA KWAMBA WEWE NDO UMEWAKOSEA
HILO GARI NILILONUNUA TULIENDA WOTE SHOW ROOM AU ULINILETEA NA KADI ISIOKUWA NA JINA LANGU ?? .
NA HIO NYUMBA NILINUNUA KIWANJA NIKAANZA KUJENGA ?? AU BAADA YA WEWE KUTUPELEKA KATIKA NYUMBA ULIZOWAJENGEA KAKA ZANGU UKANIONESHA MSINGI AMBAO ULIANZA KUJENGA ALAF UKANIAMBIA ETI UTAMALIZIA
 (VIDEO SOUTH AFRICA)
ULISEMA MADAM AMEJITOLEA KUFANYA YEYE KAMA YEYE KWA SABABU ALITAKA MSANII ANAETOKA KATIKA SHINDANO LAKE AFANYE VIZURI PIA KATIKA GEM YA BONGO FLEVA .


NAONA HAYO NDO UNAYOYAHESABU KATIKA MILIONI 50 ZETU BABA MLEZI 

NASHKURU *BSS NA MADAM RITHA KWA KUNIFANYA KUWA KAYUMBA NA SITOACHA KUSHKURU PIA WOOTE MLIOCHANGIA MIMI KUWA HAPA NAWAHESHIM SANA NA SITOACHA KUWAHESHIM DAIMA
Haikupita muda Mkubwa Fella akaweka Comment yake iliyosomeka hivi.

Mwanangu upepo huo toa ngoma.
Kijana Kayumba akajibu
"Sitowi ngoma kwa upepo wa kisurisuri.

JE, UNADHANI KUNA UMAHIMU WA KUFUATILIA HAKI ZA WASANII HAWA WOTE ILI KUJUA UNDANI??

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Falla Mkubwa, na mchongo wote wa Kitapeli ndio maana Salama Bint Jabir akaamua kusepa, nyie na Dhambi zenuu,
    Huoni hata haya Wewe Rita uvae mawigi ya bei mbaya baada ya kudhulumu hawa wanyonge.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad