KENYA imetangaza kuwa itaanza kufungua hoteli ila ni zile tu ambazo wahudumu wake watakuwa wamefanyiwa vipimo kubaini iwapo hawana Ugonjwa wa COVID 19.
Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe anasema kuwa hoteli hizo zitahitajika kufuata kanuni kama vile kuhakikisha kuwa hakuna misongamano katika hoteli hizo.
Wizara ya Elimu nchini Kenya imetangaza shule nchini humo kuendelea kufungwa hadi Juni 4 mwaka huu kutokana na idadi ya wagonjwa wenye virusi vya Corona kuongezeka. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu nchini humo Profesa George Magoha.
Wakati huo huo idadi ya watu waliopona virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 114 baada ya watu 8 zaidi kuruhusiwa kuondoka hospitalini.
Waziri wa afya aidha anasema kuwa idadi ya waliothibitishwa kuwa na virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 363 baada ya visa 8 zaidi kuripotiwa.
Wagonjwa wanne wakiwa hapa Nairobi na 4 kaunti ya Mombasa. Wangonjwa wote 8 wapya wakiwa ni raia wa Kenya.