Kenya yajibu Kuhusu Kufanyiwa Majaribio ya Chanjo ya Corona


Serikali ya Kenya imesema haifahamu mpango wowote juu ya kufanyiwa majaribio ya chanjo ya virusi vya Corona na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza.



Akizungumza Ijumaa, Aprili 24, mtaalam wa tahadhari za afya wa Serikali, Rashid Aman amesema kuwa Serikali ya Kenya haijapokea taarifa yoyote kuhusu mpango huo.

"Hatuna taarifa yoyote kuhusu hili mpaka sasa, lakini kama ikitokea basi taratibu lazima zitafuatwa. Hao watafiti wa Oxford ni lazima waishirikishe Serikali ya Kenya na baada ya hapo taratibu zitafuatwa ikiwemo chanjo hiyo kuthibitishwa na Bodi ya Uthibiti wa Madawa na Sumu", amesema Rashid Aman.

Watafiti hao wamesema kuwa watatafuta mbadala wa majaribio ya chanjo hiyo endapo haitaleta matokeo ya haraka nchini Uingereza, wakiitanja Kenya kuwa ni mojawapo ya nchi iliyo katika mbadala wao.

Mtandao wa BBC, umesema kuwa watafiri hao watafanya majiribio ya chanjo mbili, ambapo kundi la kwanza watajaribiwa chanjo ya COVID-19 na kundi lingine watajaribiwa chanjo ya ugonjwa wa 'Meningitis' lakini majibu yake yatajulikana katika miezi kadhaa ya baadaye.

Idadi ya maambukizi ya COVID-19 mpaka kufikia Aprili 25 ni 2,809,979, waliopona wakifikia 789,069 huku idadi ya vifo ikifikia 197,006, hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Al jazeera.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad