Kiba: Sykes Ndo Aliyenitambulisha Kwenye Muziki





MFALME wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba amevunja ukimya na kufunguka kuhusu namna ambavyo msanii mwenzake, Dully Sykes alivyoshiriki katika kumnyanyua kimuziki kwa kutengeneza wimbo wake wa kwanza mwaka 2003.

Kiba kupitia Insta Live yake amesema Dully Sykes alimsikia akiimba kwa mjomba wake, akapenda sauti, akamchukua na kwenda studio kwa Enrico na wakarekodi wimbo wa Kuteseka Nimechoka. Baada ya hapo Dully Sykes alimtambulisha Alikiba kwa G Lover na kuanzia hapo Alikiba akaanza kufahamika.

Hata hivyo Kiba amewashukuru wale wote waliomshika mkono katika safari yake ya maisha wakiwemo, Mully B, Prof. Jay, Sugu, Dj. Venture, pamoja na Dj Majey aliyekuwa Dj wa kwanza kuchukua CD yake na kumpambania wimbo wake kupigwa.

King Kiba pia awamewataka mashabiki wake kuendelea kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kufuata maagizo ya mamlaka husika huku akiwataka kukaa mkao wa kula kwasababu Alhamis wiki hii anadodosha wimbo mpya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad