Kigwangalla Ajibu Matumizi ya Bilioni 2 Kinyume na Utaratibu


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewajibu wanaomsakama katika mitandao ya kijamii wakitaka awajibike  baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania (CAG) kubaini  matumizi ya Sh2.58 bilioni yaliyofanywa na wizara hiyo  nje ya bajeti na kabla ya kupitishwa na Bunge.

Katika majibu yake katika mtandao wa kijamii wa Twitter, Dk Kigwangalla amesema haogopi kutumbuliwa, kuwataka wahusika kusubiri muda muafaka wa ripoti hiyo kujadiliwa bungeni ili kujua ukweli na kusisitiza kuwa wakati ukaguzi huo unafanyika alikuwa amelazwa hospitali na ana amini timu ya wizara hiyo ilifuata utaratibu.

Ripoti kuu ya mwaka kuhusu ukaguzi wa taarifa za fedha za Serikali kuu kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2019, ilieleza matumizi ya Sh2.58 bilioni yaliyofanywa na Wizara hiyo nje ya bajeti na kabla ya kupitishwa na Bunge.

Fedha hizo zimetumika kufanikisha kampeni ya Urithi Festival Celebration and Channel maalum ya kutangaza vivutio vya utalii kinyume na taratibu.

 “Nilipitia matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kubaini kiasi cha Sh2.58 bilioni kimetumika kuanzisha chaneli ya Televisioni “Urithi Festival” ili kutangaza vivutio vya utalii,” imeeleza ripoti hiyo.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Khamis, Mitandao mwachie Godiless na genge lake.

    Dhamira zao zinajulikana na time frame ya matukio na uamuzi pia tunaendelea kuuchambua.

    Wasikupe stresi naww kujiunga katika twitter na facebook. HAWANA JINGINE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad