Kim Jong Ameenda Kusikojulikana Kujitibu- Ikulu ya Korea Kusini Yafunguka
0
April 21, 2020
Serikali ya Korea Kusini imesema kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anaonekana kuendelea kuongoza shughuli za serikali kama kawaida, baada ya uvumi usio na uthibitisho kusema kuwa yuko katika hali dhaifu baada ya kufanyiwa upasuaji.
Ikulu ya Korea Kusini imesema hakuna tukio lolote lisilo la kawaida ambalo limegundulika Korea Kaskazini na kuwa haina habari yoyote kuhusu uvumi huo kuhusu afya ya Kim.
Ikulu ya Korea Kusini imesema Kim anaaminika kuwa katika eneo lisilojulikana nje ya mji mkuu Pyongyang akiwa na watu wake wa karibu.
Katibu wa Baraza la mawaziri la Japan Yoshihide Suda amesema wanafuatilia habari hizo kwa karibu: vumi mara nyingi huibuka kuhusu uongozi wa Korea Kaskazini kwa kuzingatia uhudhuriaji wa hafla muhimu za serikali.
Kim, mwenye umri wa miaka 36, hakuhudhuria sherehe ya marehemu babu yake na muanzilishi wa taifa Kim Il Sung mnamo Aprili 15, ambayo ni sikukuu muhimu kabisa ya nchi hiyo.
Tags