Kim Nana Atamba Kuwaziba Watu Midomo



MUUZA nyago kunako video za Bongo Fleva, Lilian Kessy ‘Kim Nana’ ambaye alikwaa skendo ya kutoka kimapenzi na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Mondi’ ametamba kuwaziba watu midomo baada ya kumposti mtoto wake kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa kijamii.

Kim Nana ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, alipokuwa mjamzito watu kwenye mitandao waliongea wanavyotaka kuhusu baba wa mtoto, lakini ukweli ulibaki kwake.

“Mtoto wangu amefikisha siku arobaini, namshukuru sana Mungu, nimeweka picha yake kwenye ukurasa wangu wa Instagram ili kuziba vizavizabina ambao walikuwa wakinizungumzia vibaya, mara sijui nimezaa na Diamond (Mondi) sasa waingalie hiyo sura wataacha kuongea mambo ya watu hovyo,” amesema Kim Nana.

Wakati Kim Nana akiwa mjamzito habari ziliibuka kuwa ni wa Mondi na siyo wa mpenzi wake ambay ni mtangazaji T-Bway.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad