Kinachoendelea kuhusu kifo cha mama Rwakatare



Familia ya Askofu Dr. Gertrude Rwakatare, imesema kuwa kwa sasa bado inasubiri taratibu za kikao cha familia pamoja na Serikali kabla ya kutoa taarifa kuhusu msiba huo.

Mtoto wa marehemu ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kawe Mkoani Dar es salaam, Bw. Muta Lwakatare, amewaasa wapendwa wa marehemu mama yake kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho taratibu zinasubiriwa.

Amesema kuwa watu wanaweza kufika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kutoa pole, lakini ni kwa utaratibu maalum wa kuepuka mikusanyiko ikiwa ni hatua za kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya Corona.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku moja imepita tangu kifo cha Mchungaji na Askofu wa Kanisa la Mlima wa Moto, Dr. Gertrude Rwakatare kilichotokea Alfajiri ya jana Aprili 20, katika Hosptali ya Rabininsia jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad