Kitendawili cha Mbunge Kubenea Kung’oka au Kubaki Chadema Kitateguliwa Kesho



Baada ya mwezake Antony Komu (Mbunge wa Chadema moshi vijijini) kutangaza kung’atuka ndani ya Chadema na kujiunga na Chama cha NCCR Mageuzi Mbunge wa Chadema Jimbo la Ubungo Saed Kubenea anatarajia kuwa na mkutano wa waandishi wa habari.

Itakumbukwa kuwa Oktoba, 2018, Komu na Kubenea ni marafiki na mara kadhaa wamepewa adhabu ya pamoja kwa kosa kuunda njama ovu dhidi ya mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe na Meya wa Ubungo Boniphace Jacob.

Wabunge Chadema wazungumzia madai ya kuvuja kwa sauti zao ...

Siku chache zilizopita Komu aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kutangaza uamzi wake na kesho Kubenea ataongea na wanahabari hajeleza ni nini hasa atazungumzia lakini watu wameanza kunong’ona kuwa huenda akangatuka katika chama chake cha sasa.

Komu na Kubenea wamekuwa wakihusishwa kuondoka Chadema kwa muda mrefu mmoja kati yao ameskwisha tangaza nia mwingine haifahamiki pengine kusubiri kesho.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad