Kwanini Ulaya na Amerika Wengi Wamefariki Kwa Corona Kuliko Afrika...Wadau Watoa Sababu



Huku janga la virusi vya korona likizidi kuwa donda ndugu kote duniani, imebeinika kuwa virusi hivyo vimeathiri pakubwa nchi za Uzunguni kuliko Afrika.

Visa vya maambukizi na idadi ya vifo vilivyoripotiwa katika nchi hizo vimewaacha wengi vinywa wazi ikikumbukwa kwamba wao ndio wana miundo misingi imara zaidi ya kuweza kudhibiti majanga ikilinganishwa na Afrika.

Swali hili lilimsumbua bwana mmoja aliyeamua kujimwaya mtandaoni kuuliza kinachofanya Afrika kuweza kudhibiti virusi hivyo licha ya kukosa teknolojia ya kupambana na majanga kama hayo.

”Mbona hawa watu hawafi? Ni nini tulikosea kufanya ifaavyo? Weffrey Jellington aliuliza katika ukurasa wa twitter.

Baada ya muda mfupi tu, watu wa kila tabaka walijimwaya mitandaoni kumpa majibu.

Baadhi walidai kuwa tangu kukurupuka kwa virusi hivyo, tofauti ni kuwa Waamerika wamekuwa wakifanya kila wawezalo kukabiliana nalo huku Waaafrika wakiamini kuwa Mungu tu ndiye suluhu pekee wa kuweza kuwaepuka na janga hilo.

Baadhi ya walidai kuwa Waafrika ni magwiji katika mambo ya ushirikina na uganga na ndiyo huweza kuwakinga pakubwa.

Wengine walisema kuwa maisha ya mateso na umaskini ambayo waafrika hupitia huimarisha kinga ya miili yao na hivyo si rahisi kuambukizwa virusi hivyo.

Hizi hapa ni baadhi ya jumbe hizo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad