Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema amemshauri Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupiga marufuku safari za mazishi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
“@umwaliku safari za mazishi kutoka sehemu moja kwenda nyingine ziratibiwe au zipigwe marufuku kwani zaweza kuwa chanzo cha maambukizi Covid 19 vijijini,”.
Lema aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter huku akisema kuwa Tanzania mazishi ni heshima na watu wanasafiri kutoka sehemu mbalimbali za nchi hasa jamii zenye utamaduni wa kuzika kwao.
@umwalimu Safari za mazishi kutoka sehemu moja kwenda nyingine ziratibiwe au zipigwe marufuku kwani zaweza kuwa chanzo cha maambukizi Covid 19 Vijijini.Tanzania mazishi ni heshima na watu wana safiri kutoka sehemu mbali mbali za Nchi haswa kwa Jamii zenye utamuduni wa kuzika kwao— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) April 20, 2020