Mbunge wa Arusha mjiji (Chadema), Godbless Lema, amesema Kenya kuanzia sasa madaktari na wauguzi wanao hudumia wagonjwa wa virusi vya Corona wamepatiwa nyumba na kujitenga na familia zao.
Lema amesema nyumba hizo zinagharamiwa na serikali ili kulinfa familia zao na maambukizi ya ugonjwa huo.
Lema aliandika ujumbe huo katika ukurasa wa Twitter kuwa ni utaratibu wa maana uliojaa upendo ” Tufikiri namna hii pia,”
Aliandika ujumbe huu
“@umwalimu @MagufuliJP Kenya kuanzia sasa madaktari na wauguzi wanao wahudumia wagonjwa wa Corona virus watakuwa wanaishi nje ya nyumba zao kwa gharama ya serikali ili kulinda familia zao na maambukizi ya ugonjwa huu. Ni utaratibu wa maana uliojaa upendo. Tufikiri namna hii pia,”
@umwalimu @MagufuliJP Kenya kuanzia sasa Madaktari na Wauguzi wanao wahudumia wagonjwa wa Corona virus watakuwa wanaishi nje ya nyumba zao kwa gharama ya Serikali ili kulinda familia zao na maambukizi ya ugonjwa huu. Ni utaratibu wa maana uliojaa upendo.Tufikiri namna hii pia.— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) April 7, 2020