Limao Katika Mwili wa Binadamu Huongeza Kinga ya Mwili


Tafiti zimebainisha kuwa mtu anashauriwa kutumia maganda ya ndimu kama ambavyo anatumia juisi ya limao kwani maganda hayo yanavirutubisho muhimu sana katika mwili wa binadamu hasa katika kupambana na kiwango cha sukari ndani ya mwili.

Matumizi ya Limao katika mwili wa binadamu huongeza kinga mwilini ya kupigana na magonjwa mbalimbali, na ndio maana inashauriwa kwa wale wenye kinga pungufu dhidi ya magonjwa kutumia limao ili kuipa nguvu kinga ya mwili kupingana na magonjwa mbalimbali.

Aidha, utumiaji wa juisi ya limao kila siku asubuhi una faida kubwa sana katika mwili wa binadamu, kwani limao lina virutubisho na madini mbalimbali kama Calcium, Magnesiam, vitamin C, Zink, Potasiam, kopa, chuma na Protini.

Limao husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kulainisha choo, hivyo kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo la kupata haja kubwa wanashauriwa kila siku asubuhi kutumia juisi ya limao ili kusaidia kupata haja kubwa kwa urahisi.

Matumizi ya limao hutunza mfumo wa kinywa hasa kwa kujali afya ya meno, utumiaji wa limao kila siku asubuhi husaidia kubadilisha rangi ya meno yako hasa wale wenye meno ya njano ndimu husaidia kung’arisha meno nakuyafanya yawe katika hali ya kawaida ya uweupe.

Hata hivyo katika urembo limao hukuza nywele, inashauriwa wakati mwingine kuchukua kiasi fulani cha ndimu na kupaka katika nywele hii husaidia kufanya nywele zako kuwa zenye afya na kwa wale wenye nywele chache limao husaidia kujaza nywele na kuzing’arisha na kuzifanya zipate muonekano wa asilia.

Licha ya limao kuwa na uchachu mdomoni pia husaidia kupunguza uzito  wa mwili, madaktari wanasisitiza kila asubuhi mtu kutumia glasi ya maji yaliyochanganywa na ndimu pamoja na asali husaidia mfumo wa kuyeyusha mafuta ndani ya mwili na kumfanya mtu apunguze uzito.

Aidha matumizi ya Limao husaidia kuepusha kupata uvimbe kwenye figo kwani ndimu inamiliki virutubisho ambavyo huzuia figo kuathirika na uvimbe, pia limao katika mwilini hufanya kazi ya kuchuja sumu katika ini na figo kutokana na kazi yake ya kusafisha vijidudu vyote vinavyosababisha bacteria wabaya mwilini.

Matumizi ya Limao huongeza kinga mwilini ya kupigana na magonjwa mbalimbali, na ndio maana inashauriwa kwa wale wenye kinga pungufu dhidi ya magonjwa kutumia limao ili kuipa nguvu kinga ya mwili kupingana na magonjwa mbalimbali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad