Zipo list kibao za viongozi wa dini ambazo huonesha namna gani wanakuwa na ushawishi wa kuponya watu kiroho lakini fahamu pia kuwa zipo list za viongozi hao hao wa dini ambao wanatajwa kuwa na fedha nyingi zaidi duniani…na kwa mwaka huu wa 2017 tayari ninayo list ya wachungaji 10 wanaotajwa kuwa na fedha nyingi zaidi duniani.
10. Joseph Prince.
Dola Milioni 5 Ni Mchungaji kutoka Singapore ambaye anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani Milioni 5. Mchungaji Joseph hufanya ibada ambazo pia hurushwa LIVE kwenye mtandao wa youtube hivyo kupata umaarufu mkubwa sana barani Asia na duniani.
9. T.B Joshua
Dola Milioni 10 Ni mzaliwa wa Nigeria na anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani Milioni 10. Kwa Nigeria, mchungaji huyu ni maarufu kama Nabii na ana watu wanaomfuatilia kwenye mtandao wa Facebook zaidi ya Milioni 1.5.
8. Billy Graham
Dola Milioni 25 Huyu ni mchungaji wa Marekani na moja kati ya wachungaji wenye umri mkubwa. Alizaliwa mwaka 1918 na kusomea masomo Anthropolojia na Biblia. Anaripotiwa kuwa na waumini wanaomfuatilia zaidi ya Bilioni 2.2 na utajiri wa Dola za Kimarekani Milioni 25.
7. Kenneth Copeland
Dola Milioni 25 Anafahamika sana kwa ujumbe mkubwa wa mahubiri yake ambayo ni mafanikio na utoshelevu. Kabla ya kuwa Mkristo alikua mwanamuziki kazi iliyompa mafanikio makubwa. Moja ya nyimbo zake ni pamoja na “Pledge of Love” alioufanya mwaka 1957 na kuingia kwenye chat bora za Billboard kwa kushika namba 17. Yeye na familia yake wanaishi katika nyumba yenye gharama ya Dola Milioni 6.3
6. Creflo Dollar
Dola Milioni 27 Ni Mchungaji wa Marekani, na kama jina lake lilivyo, Mchungai huyu anamiliki gari ya thamani aina ya Rolls Royce, na nyumba tatu za gharama ya Dola Milioni 2.5. Mwaka 2013 alishitakiwa kwa kosa la kumshambulia mwanaye wa kike lakini baadaye kesi hiyo kuachwa kwa madai ya kutatua kifamilia.
5. Enock Adeboye
Dola Milioni 39 Mchungaji huyu yuko Nigeria. Kanisa lake la Redeemed Christian Church of God lina matawi 14, 000 ndani ya Nigeria pekee na katika nchi nyingine zaidi ya 100 nje ya nchi hiyo. Image result for Enoch Adeboye.
4. Benny Hinn
Dola Milioni 42 Mchungaji huyu pia ni Mmarekani. Mafundisho yake ni kuhusu imani na uponyaji. Anaripotiwa kuwahi kuchunguzwa na Serikali ya nchi hiyo kwa kashfa za kutolipa kodi.
3. Chris Oyakhilome.
Dola Milioni 50 Mchungaji Chris ni miongoni mwa wahungaji matajiri kutoka Afrika ambaye anatokea Afrika Kusini. Tofauti na kuwa na waumini wengi kwenye matawi ya Kanisa lake mchungaji huyu pia anamiliki matawi ya kazi za misaada na elimu. Anamiliki vituo vitatu vya Televisheni ambavyo vinapata waangaliaji hadi Milioni 2.5 kila siku.
2. Bishop T.D. Jakes.
Dola Milioni 147 Askofu huyu anatokea Marekani na anaongoza Kanisa la Potter’s House. Amewahi kuonekana na Maraisi wa Marekani George Bush na Barack Obama ambao kwa nyakati tofauti wamemsifia mchungaji huyo kwa kuwa mwaminifu.
1. Bishop David Oyedepo
Dola Milioni 150 Huyu ndiye Mchungaji tajiri kuliko wote duniani ambaye anamiliki Kanisa lijulikanalo kama Winners Chapel. Kanisa lake lina matawi katika nchi 45 barani Afrika ikiwa ni pamoja na mengine nchini Dubai, Uingereza na Marekani.
List ya Wachungaji Matajiri zaidi Duniani 2017 hii hapa
0
April 02, 2020
Tags