BAADA ya kushambuliwa kwa kutomposti mtoto wa mpenzi wake, Francis Ciza ‘Majizo’ aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto aitwaye Baby Fansy, staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa waraka mzito.
Wikiendi iliyopita, Baby Fansy alikuwa akitimiza umri wa miaka mitano, lakini Lulu hakumtakia heri ya siku ya kuzaliwa, jambo lililoibua mjadala kama wote kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya kuona anazidi kushambuliwa, Lulu alitoa waraka huo kupitia mitandao ya kijamii ambapo ameeleza ya moyoni mwake.
“Nimeelewa ni kiasi gani watu tumeruhusu mitandao ichukue zile akili za kuzaliwa kabisa. Labda nijaribu ku-share jambo kwa huu uelewa wangu mdogo nilionao, kuposti mtu mtandaoni haimaanishi upendo kama wengi wetu tunavyochukulia, kuposti ni jambo la ziada tu.
“Kwa mfano unamposti mtoto wa miaka mitano ambaye hata Instagram haijui, unafikiri ndiyo njia anayoweza kuhisi upendo wako? Sisemi kwamba haitakiwi au tusifanye, unaweza kuamua kufanya au kutokufanya kwa sababu ni ziada tu.”
Kuhusu ishu hiyo, Mobeto yeye alijibu kwa kifupi; “Ni kweli mwanangu ametimiza miaka mitano, hata Lulu angemposti mwanangu ni sawa tu, ningeona kitu cha kawaida japo sisi tunaichukulia tofauti kwenye mitandao ya kijamii.”
STORI: NEEMA ADRIAN, DAR
GPL