Madam Ritha akalia kuti kavu, Serikali yampa mwezi mmoja kumlipa mshindi wa BSS milioni 50




NAIBU Waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo, Juliana Shonza, leo Aprili 08, anazungumza jijini Dodoma kuhusiana na mshindi wa Bongo Star Search (2019) Meshack Fukuta, kutolipwa fedha zakena kumpa mwezi mmoja Madam Ritha kumlipa pesa hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri Shonza amesema yeye ndio alikuwa mgeni rasmi wa fainali hizo na mshindi alitakiwa kupata milioni 50 ambazo milioni 20 kwaajili ya mshindi na milioni 30 zitatumika kwaajili ya kummeneji ikiwa ni pamoja na kumpeleka studio kurekodi nyimbo na video.

"Kwkuwa BBS wamesema wana milioni thelathini za kummeneji Meshack sasa hatujui watammeneji kwa namna gani sasa tunawataka BSS watuletee mkataba wa mpango kazi wao ambao wameupanga kwa namna wanavyoweza kummeneji waonyeshe gharama za kumpeleka studio, kama kuna kumpeleka chuo cha muziki tuone kila kitu kiwe kwenye mkataba ili tuone thamani ya hela iliyotumika kwa mwaka" alisema waziri shonza

Sisi kama wizara tumepokea barua ya malalamiko kutoka kwa wazazi wa meshaki kutokana na kutirizishwa na mtoto wao alivyotendewa ni kweli ana malalamiko makubwa hajalipwa pesa zake sasa unaenda mwezi wa nne mwenyewe  pamoja na wazazi wamekuwa wakifuatilia bila mafanikio yeyote"

Waziri Shonza amesimulia ujanja aliouona siku ya fainali ya mshindi wa BSS na kusema kuwa "nakuta mnajiuliza kwanini serikali imekuwa kimya kwa muda wote huo ila serikali aiwezi kuwa mlalamikaji bali ni muhusika mwenyewe atakapolalamika ndio tunachukua hatua"

Pia amesema  hata siku yenyewe ya tukio ilionekana ni uhuni kwakuwa yeye alikuwa ni mgeni rasmi na alitakiwa kutoa zawadi kwa mshindi lakini siku ile haikuwa hivyo.

"Baada ya kupokea malalamiko wizara ikamtafuta mkurugenzi wa Benchmark Madam Ritha Paulsen ambapo amekiri kweli hawajamlipa milioni hamsini na amesema kuwa hayo yote yametokea kutokana na changamoto ya udhamini kwakuwa bado hawajalipwa lakini sabau zake hazina mashiko kwakuwa tuliwatafuta Star media ambao ni wadhamini na kusema kuwa wamelipwa pesa zote.

Sasa tunaona kuwa kuna mazingira ambayo ya sintofahamu utetezi wake alioutoa si kweli ni uongo na kwa namna hii sisi kama wizara hatuta lifumbia macho kwa sababu kwa namna nyingine walinialika mimi kama naibu waziri kuwa mgeni rasmi  ila ntaonekana na mimi nimeshiriki katika kitu ambacho si halali na sisi kama wizara tumesikitika kwakua wamekiuka sheria.

Baada ya kubaini kuwa Madam Ritha amedanganya na kuna ujanja mkubwa uliofanyika maelezo ya serikali ni haya madam ritha ameomba mwenzi mmoja ili aweze kumlipa serikali tumekubali na tunamlipa na kama akikiuka haya tena tutayafungia hayo mashindano

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii ni pesa Mbuzi kwa Madam Rita.
    gauni lake ml 3 nywele bandia mil2 kiatu mil4 handibegi mil7 saa mil5 mkufu na pete mil12 gari mil70.

    Check ya pesa za mshindi ikifanikiwa kesho tutaidepoziti.

    Star Media kama vp mmemalizana poa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad