Magufuli: asamehe wafungwa 3,973 , atoa ujumbe kuhusu Corona



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewatakia heri Watanzania wote katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Amewataka Watanzania kutumia siku ya kesho Aprili 26, kuutafakari Muungano ulioasisiwa na viongozi wakuu Baba wa Taifa, hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu atuepushe na janga la virusi vya Corona.

Katika kuadhimisha miaka 56 ya Muungano, Mhe. Rais Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3973, ambapo kati yao, wafungwa 3717 wamesamehewa vifungo vyao na wafungwa 256 waliokuwa wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa mpaka kufa wamebadilishiwa adhabu.

Mhe. Rais Magufuli amesema ana matumaini kuwa wafungwa hao wamejifunza na kujirekebisha ili waungane na jamii katika kulitumikia Taifa wakiwa raia wema wanaozingatia sheria.

Aidha Rais Magufuli amewakumbusha Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona, ikiwemo kujiepusha na mikusanyiko na safari zisizo za lazima.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwenyezi Mungu Akullinde JPJM.

    Msikilize khotuba ya Shk Nassor Hamza miaka sita iliyopita. Chanzo cha Matatizo ni Sisi.

    Allah akulinde wewe kwa Uadilifu.
    Nawewe ni kiongozi mteule.

    Leo Sukari mawaziri wanaitolea elekezi baada ya Mh Majaliwa kuizungumzia.

    Mungu akulindeni na kuwabariki wote.

    Hasunga / Bashungwa/ K. Majaliwa / ma DC na watendaji wako wote. tafadhalini muisikilize hii khotuba imeguia yote
    UTAWALA / JANNGA HILILA CORONA N.K

    ReplyDelete
  2. Allah akujaalie KILA LA kheri na akulinde na Mahasid wanapo husudu.

    Ramadhan Kareem.

    https://youtu.be/1K_Bkx5OnpU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad