Mahabusu Watatu Wafariki dunia Wakijaribu Kutoroka Gerezani



Na Paschal D.Lucas, Mwanza.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza ACP Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa mahabusu watatu waliokuwa wanashikiliwa kwa kesi ya mauaji na uhujumu uchumi wamefariki dunia wakati wa jaribio lao la kutoroka katika gereza la Butimba.

Amesema mnamo Aprili 14,2020 muda wa 12:30 jioni katika gereza la Butimba watuhumiwa Yusuph Benard (34) mwenye namba ya Mahabusu 3444/2016 na Seleman Seif (28) mwenye namba ya Mahabusu1177/2017, wote wakiwa na kesi ya Mauaji walijaribu kutoroka kwenye gereza hilo huku askari Magereza kwa kushirikiana na Wananchi waliwakimbiza na kufanikiwa kuwakamata.

" Wananchi wakiwa na hasira kali kutokana na kitendo hicho waliwashambulia kwa kuwapiga mahabusu hao kitendo ambacho kilipelekea hali zao kuwa mbaya hivyo Jeshi la Polisi liliwapeleka katika hospitali ya Mkoa ya Sekou-Toure kwa ajili ya Matibabu lakini ilipofika majira ya saa 8.30 mchana walifariki Dunia wakati wakiendelea kupatiwa Matibabu".

ACP Muliro amesema Mtuhumiwa wa tatu katika utoro huo anayefahamika kwa jina la George Aloyce (34) ambaye alikuwa amefungwa kwa kosa la Uhujumu uchumi hukumu ya miaka 15 huku namba yake ya Kifungo ikiwa ni 200/2019 akiwa na kifungo kingine cha kutoroka chini ya ulinzi miezi 6, baada ya kukamatwa katika jaribio hilo la kutoroka tena kwenye gereza hilo la Butimba.

Alihojiwa na Askari Polisi na kuwaeleza kuwa kama wangeweza kufanikiwa wageenda kuchukua gari Tax katika eneo la Mabatini jijini Mwanza.

Hivyo Polisi walimtaka Mfungwa huyo kwenda kuwaonyesha Dereva Tax ambaye angewasafirisha kuelekea Katoro Mkoani Geita lakini walivyoshuka kutoka kwenye gari na kuanza kutembea huku akijidai anataka kuwaonyesha dereva huyo ghafla mfungwa huyo alianza kukimbia na ndipo Askari Polisi waliokuwanae walimwamuru kusimama huku wakipiga risasi juu lakini hakutii amri hivyo Askari Polisi walimrushia risasi zilizomjeruhi miguuni na kufanikiwa kumkamata na kumpeleka katika hospitali ya Sekou-Toure ambapo baadae naye alifariki dunia.

Hata hivyo jeshi la Polisi mkoani Mwanza linatoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa taarifa zinazohusuana na uharifu ili wahusika waweze kukamatwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad